ensw

Jumapili ya tarehe 24 January, 2016, wana Parokia ya Upanga walisherehekea kwa pamoja Sikukuu ya Parokia. Sherehe hizi zilianza kwa ibada ya misa takatifu iliyoongozwa na Baba Paroko, Pd. Kavishe, Pd. Paul Mashauri, na Pd. Joachim wa shirika la Don Bosco. Ibada ya misa ilifuatiwa chakula cha mchana na burudani chache kutoka kwa watoto na vijana wa Parokia.

Karibu kwa ajili ya kusoma ripoti za utendaji wa Jumuiya za Parokia yetu mwaka 2015.

Kama ilivyo kawaida yao, kila mwaka, kwenye mkesha wa Christmas, vijana wa Parokia yetu huwa wanaigiza igizo la Kuzaliwa kwa Yesu. Utamaduni huu ulioanza mwaka 2010, umeendelea kila mwaka, kwa vijana kuzidi kuboresha igizo hilo. Kwa namna ya pekee, mwaka huu maandalizi yalikuwa mazuri mno, na wote walifurahia namna gani vijana walivyoweza kufanya igizo kwa wakati.