ensw
Super User

Super User

Suspendisse at libero porttitor nisi aliquet vulputate vitae at velit. Aliquam eget arcu magna, vel congue dui. Nunc auctor mauris tempor leo aliquam vel porta ante sodales. Nulla facilisi. In accumsan mattis odio vel luctus.

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Kuaga; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Msamaria mwema.
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. KIPAIMARA 2017: 1) Siku ya Kipaimara hapa parokiani ni Jumapil ijayo tarehe 3 September 2017. Kipaimara kitatolewa katika Misa ya saa 4.00 asubuhi. Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo atatoa Sakramenti hiyo ya Kipaimara. Tunawaomba wote tushirikiane katika maandalizi hayo.

2) Maandalizi ya kiroho ya Wanakipaimara, Wazazi na Wasimamizi yakutakuwa tarehe 2 Septemba 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi. Tunawaomba wote wafike bila kukosa.

 1. TANGAZO LA SEMINA YA MALEZI NA FAMILIA:

Kamati ya Malezi na Familia ya Halmashauri ya walei Parokia ikishirikiana na baba Paroko na Jimbo Kuu la Dar es Salaam inawatangazia waamini wote kuwa kutakuwa na semina ya malezi na Familia itakayoendeshwa hapa Parokiani siku za Jumamosi kuanzia tarehe 9/9/2017. Semina itakuwa ni ya masaa 2 kuanzia saa 9 mchana kwa muda wa miezi 3. Semina ni kwa ajili ya wanandoa wachanga, wale walioandikisha ndoa parokiani hapa na wachumba. Hata hivyo wote tunakaribishwa kwani malezi na familia ni suala linalohusu jamii yote. Tunawaalika hata wale waliohudhuria semina iliyopita lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza uhudhuria yote. Tunaweza kuwaalika hata wale ambao hawaishi kwenye maeneo ya Parokia yetu.

 1. TOKA JUMUIYA YA MT. IMAKULATA: Jumapili ya leo Jumuiya ya Mt. Imakulata wanauza chai na vitafunwa kila baada ya Misa. Mapato yatatumika kwa ajii ya matendo ya huruma. Wote tunaalikwa kuwaunga mkono.
 1. TOKA JUMUIYA YA MT. YUDA THADEI: JUMBLE SALE!!

Jumuiya ya Mt. Yuda Thadei, kwa mara nyingine inakualika kwenye Jumble Sale itakayofanyika siku za Tarehe 09 na 10 September 2017 kuanzia saa mbili asubuhi. Jumble Sale itafanyika nyumba na 412, Barabara ya Umoja wa Mataifa (kwa familia ya Mwenda, pale kwenye Keki). Jumble Sale ni nafasi ya pekee sana kupata vitu vizuri sana kwa bei nafuu kuliko kawaida. Karibuni sana, karibuni wote.

 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru jumuiya ya Mt. Yuda Thadei kwa kutuchangia kiasi cha shilingi laki moja baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita.

2) Leo mara baada ya Misa ya tatu vijana tutakuwa na ibada ya kuabudu EKARISTI TAKATIFU. Vijana wote mnakaribishwa.

3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda B na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda C. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya MAGDALENA WA CANOSSA. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Petro. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. KUAGA: Tunamuaga Paroko msaidizi Fr. Augustine Olomy ambaye amepata uhamisho kuhamia Parokia ya Mbagala Kizuiani hapa Dar es Salaam. Tunamshukuru kwa utume wake katika Parokia ya Upanga. Tunamtakia baraka katika utume wake mpya. Pia tunamuaga Br. Salvatory Nkalango ambaye amepata uhamisho wa kwenda kwenye nyumba yetu kuu – Msimbazi. Tunawatakia wote baraka za Mungu na maisha mema.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I: Ndugu GASPER RICHARD ABDALAH mwana wa Richard Abdalah na Mama Anna Solomon wa KKKT Machame – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi PHILIPINA LEONARD LYAKURWA binti Leonard Mshabaa na Mama Donasia Seneli wa Mengwe – Moshi. Ndoa ni tarehe 14/10/2017.

TANGAZO II:

Ndugu ISAAC TITUS CHANZI mwana wa Titus Chanzi na Mama Rosemary Chanzi wa Muhimbili, anatarajia kufunga ndoa na Bi DINA SADA NGOSHANI binti Mmadi Ngoshani na Mama Pauline Ngoshani wa Kijitonyama. Ndoa ni tarehe 11/11/2017.

Ndugu ELIAS mwana wa Zakaria Mabula na Mama Agnes Tindosi wa Mt. Ambros Taghaste, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAZINAEL binti George Mchomvu na Mama Sensia Greyson wa Mt. Ambros Taghaste. Ndoa ni January 2018.

TANGAZO III

Ndugu DEOGRATIUS LAZARI mwana wa Lazaro Ndesingo (sasa marehemu) na MamaAurea Ndesario wa Kilema – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi BORA OMARY binti Omary Hamisa Ndanyungu (sasa marehemu) na Mama Siya Leonard Mkama wa Kigoma. Ndoa ni tarehe 7/10/2017.

Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hizi atoe taarifa ofisini kwa Paroko.

“Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Ulinzi Parokiani; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Kuaga.
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. TANGAZO LA SEMINA YA MALEZI NA FAMILIA:

Kamati ya Malezi na Familia ya Halmashauri ya walei Parokia ikishirikiana na baba Paroko na Jimbo Kuu la Dar es Salaam inawatangazia waamini wote kuwa kutakuwa na semina ya malezi na Familia itakayoendeshwa hapa Parokiani siku za Jumamosi kuanzia tarehe 9/9/2017. Semina itakuwa ni ya masaa 2 kuanzia saa 9 mchana kwa muda wa miezi 3. Semina ni kwa ajili ya wanandoa wachanga, wale walioandikisha ndoa parokiani hapa na wachumba. Hata hivyo wote tunakaribishwa kwani malezi na familia ni suala linalohusu jamii yote. Tunawaalika hata wale waliohudhuria semina iliyopita lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza uhudhuria yote. Tunaweza kuwaalika hata wale ambao hawaishi kwenye maeneo ya Parokia yetu.

 1. TANGAZO LA WAWATA: Kwa upendo wa Kristo…… Kutakuwa na ziara ya Visiga kwa WAWATA wote wa Jimbo kuu la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utume wetu. Ziara itafanyika tarehe 26/8/2017. Safari itaanza Parokiani saa 12.00 asubuhi. WAWATA wote wanaombwa kuhudhuria kwa kujiandikisha mapema kwa viongozi au kwa Masista. Michango yote imetolewa kupitia Jumuiya, hivyo hakutakuwa na michango mingine ya safari. Tunawatakia utume mwema.
 1. TOKA JUMUIYA YA MT. IMAKULATA: 1) Watakutana leo mara baada ya Misa ya pili kwenye ukumbi wa vijana. Wanajumuiya wote wanahimizwa kushiriki,

2) Jumapili ijayo Jumuiya ya Mt. Imakulata watauza chai na vitafunwa kila baada ya Misa. Mapato yatatumika kwa ajii ya matendo ya huruma. Wote tunaalikwa kuwaunga mkono.

 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru Jumuiya ya Mtakatifu Augustino kwa kutuchangia kiasi cha shilingi elfu 50 baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita.

2) Leo vijana tutaangalia movie ya maisha ya Mtakatifu PIO Yenye mafunzo mbalimbali Vijana wote tunakaribishwa.

3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda A na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda B. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya YUDA THADEY. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Magdalena wa Canossa. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. UHAMISHO: Paroko msaidizi Fr. Augustine Olomy amepata uhamisho kuhamia Parokia ya Kizuiani hapa Dar es Salaam. Tunamshukuru kwa utume wake katika Parokia ya Upanga. Tunamtakia baraka karika utume wake mpya. Pia Br. Salvatory amepata uhamisho wa kwenda kwenye nyumba yetu kuu – Msimbazi. Tutapata nafasi ya kuwaaga rasmi Jumapili ijayo.
 1. KUKARIBISHA: Tunafuraha kumkaribisha Ndugu Baltazar Temu ambaye amejiunga na Jamaa ya Ndugu Wakapuchini – Upanga Parokiani. Tunamkaribisha sana na kumtakia utume mwema.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I: Ndugu ISAAC TITUS CHANZI mwana wa Titus Chanzi na Mama Rosemary Chanzi wa Muhimbili, anatarajia kufunga ndoa na Bi DINA SADA NGOSHANI binti Mmadi Ngoshani na Mama Pauline Ngoshani wa Kijitonyama. Ndoa ni tarehe 11/11/2017.

Ndugu ELIAS mwana wa Zakaria Mabula na Mama Agnes Tindosi wa Mt. Ambros Taghaste, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAZINAEL binti George Mchomvu na Mama Sensia Greyson wa Mt. Ambros Taghaste. Ndoa ni January 2018.

TANGAZO II

Ndugu DEOGRATIUS LAZARI mwana wa Lazaro Ndesingo (sasa marehemu) na MamaAurea Ndesario wa Kilema – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi BORA OMARY binti Omary Hamisa Ndanyungu (sasa marehemu) na Mama Siya Leonard Mkama wa Kigoma. Ndoa ni tarehe 7/10/2017.

TANGAZO III

Ndugu JOHN GODFREY RUPIA mwana wa Steven Thomas Rupia na Mama Florah Anitha Rupia wa Anglikana, anatarajia kufunga ndoa na Bi JESSICA MWASARA binti Hussein Yusuf Mwasara na Mama Grace Simon Gumbo wa Upanga. Ndoa ni tarehe 21 October 2017.

Ndugu AMEDEUS TUKUNJOBA mwana wa Lekha Tukunjoba na Mama Joyce Nchimbi wa Kijichi, anatarajia kufunga ndoa na Bi GLORIA MUNENI binti Angelo Muneni na Mama Godliva Makoko wa Upanga. Ndoa ni tarehe 28/10/2017.

“Imani yako ni kubwa, na iwe kwako kama utakavyo.”

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Maskini na wagonjwa; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Kwaya za Parokia.
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. KOMUNIO YA KWANZA KWA LUGHA YA KIINGEREZA: Itafanyika jumapili ijayo tarehe 13 August 2017. Tunawaomba wazazi na walezi wawaandae watoto wao vizuri. Siku hiyo hakutakuwa na Misa ya watoto. Watoto wote watajiunga na watoto wenzao watakaopokea Sakramenti ya Komunio ya kwanza katika Misa ya saa 2.30.
 1. KIPAIMARA 2017: Siku ya Kipaimara hapa parokiani ni tarehe 3 September 2017. Kipaimara kitatolewa katika Misa ya saa 4.00 asubuhi. Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo atatoa Sakramenti hiyo ya Kipaimara. Tunawaomba wote tushirikiane katika maandalizi hayo.
 1. MAFUNDISHO YA KOMUNIO YA KWANZA KWA LUGHA YA KISWAHILI: Wazazi na walezi wenye watoto wenye umri wa miaka 9 na ambao hawajapa Komunio ya kwanza wafike kuwaandikisha watoto wao kwa Katekista. Wafike na cheti cha ubatizo wa watoto wao na barua ya utambulisho toka jumuiya zao.
 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru Jumuiya ya Watakatifu MASHAHIDI WA UGANDA kwa kutuchangia kiasi cha shilingi laki moja baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita. 

2) Leo mara baada Misa ya tatu vijana tutakuwa na sherehe ya kumuaga Sister Salome na kumkaribisha Sister Juliet katika ukumbi wa parokia. Vijana wote mnakaribishwa sana! 

3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda C na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda D. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. SHUKRANI: Tunamshukuru sana Sr. Salome kwa utume wake katika Parokia ya Upanga. Tunamuombea baraka za Mungu kwa utume mwingine aliopangiwa. Asanate sana na karibu tena Upanga.
 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya CAMILLUS. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Augustino. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I

Ndugu JOHN GODFREY RUPIA mwana wa Steven Thomas Rupia na Mama Florah Anitha Rupia wa Anglikana, anatarajia kufunga ndoa na Bi JESSICA MWASARA binti Hussein Yusuf Mwasara na Mama Grace Simon Gumbo wa Upanga. Ndoa ni tarehe 21 October 2017.

Ndugu AMEDEUS TUKUNJOBA mwana wa Lekha Tukunjoba na Mama Joyce Nchimbi wa Kijichi, anatarajia kufunga ndoa na Bi GLORIA MUNENI binti Angelo Muneni na Mama Godliva Makoko wa Upanga. Ndoa ni tarehe 28/10/2017.

TANGAZO II

Ndugu CHARLES KARUNGULA mwana wa January Karungula na Mama Hellen Karungula wa Upanga, anatarajia kufunga ndoa na Bi FRANCISCA SIMON binti Simon Remmy na Mama Alfredina Emmanuel wa Mabibo. Ndoa ni tarehe 9/9/2017.

Ndugu SIMON mwana wa Joseph Mutahanamilwa na Mama Alice Muta wa KKKT, anatarajia kufungu ndoa na Bi JACQUELINE binti Jackson Twissa na Mama Elizabeth Twissa wa Upanga. Ndoa ni tarehe 30/9/2017. 

TANGAZO III

Ndugu EMMANUEL MAJALIWA JANUARIUS mwana wa Januarius mkinga na Mama Amina Juma wa Kimara, anatarajia kufunga ndoa na Bi ELIZABETH KOKUZANA JASSON binti Jasson Kuamutoijo Timeishemo na Mama Paskazia Timeishemo wa KKKT Kimara. Ndoa ni tarehe 12.8.2017.

Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hizi atoe taarifa ofisini kwa Paroko.

“Huyu ni mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa naye, msikieni yeye.”

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Ukarabati Parokiani; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Maskini na wagonjwa
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. MISA YA SHUKRANI: Tunampongeza sana Fr. Benedict Shayo Paroko wa Manzese kwa Jubilei yake ya miaka 25 ya Upadre. Tukumbuke kuwa alipata ushemasi wake hapa Parokiani kwetu. Tunampongeza na kumtakia baraka za Mungu kwa utume wake.
 1. KOMUNIO YA KWANZA KWA LUGHA YA KIINGEREZA: Itafanyika jumapili ya tarehe 13 August 2017. Tunawaomba wazazi na walezi wawaandae watoto wao vizuri.
 1. KIPAIMARA 2017: Siku ya Kipaimara hapa parokiani ni tarehe 3 September 2017. Kipaimara kitatolewa katika Misa ya saa 4.00 asubuhi. Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo atatoa Sakramenti hiyo ya Kipaimara. Tunawaomba wote tushirikiane katika maandalizi hayo.
 1. KUTOKA KUNDI LA SALA LA PD PIO: Kundi la sala la Pd. Pio  tutakuwa na mkutano  Jumapili ya leo tarehe 30.7.2017 baada ya Misa ya tatu .
 1. MAFUNDISHO YA KOMUNIO YA KWANZA KWA LUGHA YA KISWAHILI: Wazazi na walezi wenye watoto wenye umri wa miaka 9 na ambao hawajapa Komunio ya kwanza wafike kuwaandikisha watoto wao kwa Katekista. Wafike na cheti cha ubatizo wa watoto wao na barua ya utambulisho toka jumuiya zao.
 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru Jumuiya ya Mtakatifu Fransisko wa Assisi kwa kutuchangia kiasi cha shilingi elfu 50 baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita. Na pia tunaomba jumuiya zinazohitaji kusaidiwa kufanya usafi na vijana watoe taarifa mapema ili vijana waweze kujiandaa mapema.

2) Jumapili ijayo tarehe 6/8/2017 mara baada ya Misa ya tatu vijana tutamuaga Sister wetu mlezi sister Salome Wanyoike pamoja na kumkaribisha Sister mpya Katika ukumbi wa vijana. Vijana wote mnakaribishwa!

3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda B na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa C. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. KUAGA: Tunamuaga Ndugu Stephano Panga ambaye alikuwa nasi kwa likizo yake ya kichungaji. Tunamshukuru sana kwa utume na kazi mbalimbali alizofanya hapa Parokiani. Tunamtakia masomo mema na baraka za Mungu katika maisha. Karibu tena Upanga.
 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya MASHAHIDI WA UGANDA. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Camillus. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I

Ndugu CHARLES KARUNGULA mwana wa January Karungula na Mama Hellen Karungula wa Upanga, anatarajia kufunga ndoa na Bi FRANCISCA SIMON binti Simon Remmy na Mama Alfredina Emmanuel wa Mabibo. Ndoa ni tarehe 9/9/2017.

Ndugu SIMON mwana wa Joseph Mutahanamilwa na Mama Alice Muta wa KKKT, anatarajia kufungu ndoa na Bi JACQUELINE binti Jackson Twissa na Mama Elizabeth Twissa wa Upanga. Ndoa ni tarehe 30/9/2017.

TANGAZO II

Ndugu EMMANUEL MAJALIWA JANUARIUS mwana wa Januarius mkinga na Mama Amina Juma wa Kimara, anatarajia kufunga ndoa na Bi ELIZABETH KOKUZANA JASSON binti Jasson Kuamutoijo Timeishemo na Mama Paskazia Timeishemo wa KKKT Kimara. Ndoa ni tarehe 12.8.2017.

Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hizi atoe taarifa ofisini kwa Paroko.

Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba.”

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Upashanaji habari; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Ukarabati Parokiani.
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. CHAMA CHA WAZEE NA WASTAAFU: Tunawaomba viongozi wa Jumuiya warudishe fomu za orodha ya wazee na wastaafu waliopo kwenye Jumuiya zao. Lengo ni kuanzisha chama cha wazee na wataafu hapa Parokiani.
 1. MISA YA SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 30/7/2017 Fr. Benedict Shayo Paroko wa Manzese kwa sasa atafika hapa kwa Misa ya kumshukuru Mungu kwa miaka 25 ya Upadre wake. Tukumbuke kuwa alipata ushemasi wake hapa parokiani kwetu.
 1. TOKA JUMUIYA YA MT. IMAKULATA: Watakuwa na mkutano wao leo mara baada ya Misa ya pili kwenye ukumbi wa Vijana. Wanajumuiya wote wanakaribishwa.
 1. MAFUNDISHO YA KOMUNIO YA KWANZA KWA LUGHA YA KISWAHILI: Wazazi na walezi wenye watoto wenye umri wa miaka 9 na ambao hawajapa Komunio ya kwanza wafike kuwaandikisha watoto wao kwa Katekista kuanzia Jumamosi ijayo tarehe 29/7/2017. Wafike na cheti cha ubatizo wa watoto wao.
 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) .Leo mara baada ya Misa ya tatu vijana tutakuwa na mada isemayo MADHARA YA UTANDAWAZI NA FAIDA ZAKE. Vijana wote mnakaribishwa na wale ambao wangependa kujifunza zaidi juu ya mada hii.

2) Tunaishukuru jumuiya ya Mtakatifu Imakulata kwa kutuchangia kiasi cha shilingi elfu 50 baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita.

3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda A na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda B. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya FRANSISKO WA ASSISI. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Wt. Mashahidi wa Uganda. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I

Ndugu EMMANUEL MAJALIWA JANUARIUS mwana wa Januarius mkinga na Mama Amina Juma wa Kimara, anatarajia kufunga ndoa na Bi ELIZABETH KOKUZANA JASSON binti Jasson Kuamutoijo Timeishemo na Mama Paskazia Timeishemo wa KKKT Kimara. Ndoa ni tarehe 12.8.2017.

Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hii atoe taarifa ofisini kwa Paroko

Neno lako ndiyo kweli Ee Bwana, Ututakase sisi kwa ile kweli.”

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Seminari ya Visiga; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Upashanaji habari.
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa. 
 1. CHAMA CHA WAZEE NA WASTAAFU: Tunawaomba viongozi wa Jumuiya warudishe fomu za orodha ya wazee na wastaafu waliopo kwenye Jumuiya zao. Lengo ni kuanzisha chama cha wazee na wataafu hapa Parokiani.
 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru Jumuiya ya Mtakatifu Monica kwa kutuchangia kiasi cha shilingi elfu 50 baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita.

2) Leo mara baada ya Misa ya tatu vijana tutakuwa na CATECHISM LESSON katika ukumbi wa vijana. Wote mnakaribishwa.

3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda D na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda A. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya IMAKULATA. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Assisi. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO III

Ndugu PATRICK JABIRI MNYONE mwana wa Paul Jabiri Mnyone na Mama Felista Patrick Chagu wa Kigamboni, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAPPY FRANK MMBAGA binti Frank Sabuni Mmbaga na Mama Edna Zebedayo Magawa wa KKKT Dodoma. Ndoa ni tarehe 26.8.2017.

Ndugu BENJAMINE KILOBA DOTTO mwana wa Musa Kiloba Dotto na Mama Lois Misuka Mnyashi (sasa marehemu) wa Shinyanga, anatarajia kufunga ndoa na Bi CATHERINE GERALD MKUDE binti Gerald Mkude na Mama Zawadi Madawili wa Upanga. Ndoa ni tarehe 29.7.2017.

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Maskini na wagonjwa; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Seminari ya Visiga.
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. CHAMA CHA WAZEE NA WASTAAFU: Tunawaomba viongozi wa Jumuiya warudishe fomu za orodha ya wazee na wastaafu waliopo kwenye Jumuiya zao. Lengo ni kuanzisha chama cha wazee na wataafu hapa Parokiani.
 1. KOMUNIO YA KWANZA KWA LUGHA YA KIINGEREZA : Wazazi na walezi wa watoto wanaofuata mafundisho ya Komunio ya Kwanza kwa lugha ya Kiingerza watakuwa na mkutano Jumamosi ijayo tarehe 15.7.2017 saa 3.00 kamili hapa Parokiani. Pia siku hiyo vijana wao watafanya mtihani kuanzia saa 2.30. vijana watakaofaulu mitihani huo watapokea Komunio ya kwanza Jumapili ya tarehe 13.8.2017.
 1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Leo mara baada ya Misa ya tatu vijana tutakuwa na ibada ya kuabudu EKARISTI TAKATIFU. Vijana wote mnakaribishwa na wale ambao wanapenda kuungana na sisi mnakaribishwa.

2) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda C na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda D. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya MONICA. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Imakulata. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO II

Ndugu PATRICK JABIRI MNYONE mwana wa Paul Jabiri Mnyone na Mama Felista Patrick Chagu wa Kigamboni, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAPPY FRANK MMBAGA binti Frank Sabuni Mmbaga na Mama Edna Zebedayo Magawa wa KKKT Dodoma. Ndoa ni tarehe 26.8.2017.

Ndugu BENJAMINE KILOBA DOTTO mwana wa Musa Kiloba Dotto na Mama Lois Misuka Mnyashi (sasa marehemu) wa Shinyanga, anatarajia kufunga ndoa na Bi CATHERINE GERALD MKUDE binti Gerald Mkude na Mama Zawadi Madawili wa Upanga. Ndoa ni tarehe 29.7.2017.

TANGAZO III

Ndugu AUGUSTINO KAWAWENARUWA mwana wa Joakimu Kilasara na Mama Maria Mawazo wa Bunju, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAPPY binti Meshack Kambey na Mama Elizabeth Mathayo wa Bunju. Ndoa ni tarehe 22.7.2017.

Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hizi atoe taarifa ofisini kwa Paroko.

“Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia.”

 1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya St. Peter’s pence; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya UWAKA (Ujenzi wa Grotto Pugu).
 1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
 1. TANGAZO LA SEMINA YA MALEZI NA FAMILIA:

Semina ya malezi na Familia inaendelea hapa Parokiani siku za Jumamosi kuanzia kuanzia saa 9.00 – 11.00 alasiri. Semina ni kwa ajili ya wanandoa wachanga, wale walioandikisha ndoa parokiani hapa na wachumba. Hata hivyo wote tunakaribishwa kwani malezi na familia ni suala linalohusu jamii yote. Tunaweza kuwaalika hata wale ambao hawaishi kwenye maeneo ya Parokia yetu.

 1. CHAMA CHA WAZEE NA WASTAAFU: Tunawaomba viongozi wa Jumuiya wachukue bahasha nyuma ya Kanisa na watusaidie kuorodhesha wazee na wastaafu waliopo kwenye Jumuiya zao. Lengo ni kuanzisha chama cha wazee na wataafu hapa Parokiani.
 1. TOKA JUMUIYA YA MT. IMAKULATA: Watakutana kwenye ukumbi wa vijana leo baada ya Misa ya pili.
 1. TANGAZO LA UWAKA: Mmoja ya majukumu waliopewa UWAKA ni kujenga na kutunza kituo cha hija cha jimbo letu huko kibaha. Kazi inaendelea na gharama ni kubwa. Katika jitihada kupata fedha za kukidhi gharama hizi, kila parokia inatakiwa ichangie Sh. Millioni tano. Tunawaomba wanaume wote wakatoliki na waumini wote  kwa ujumla kushiriki katika kuendeleza ujenzi wa kituo hiki kwa kutoa mchango wao Jumapili ijayo tarehe  2 July. Mchango wako unahitajika sana na Mungu atakubariki.
 1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya FAMILIA TAKATIFU. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Yohane mbatizaji. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
 1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I

Ndugu AUGUSTINO KAWAWENARUWA mwana wa Joakimu Kilasara na Mama Maria Mawazo wa Bunju, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAPPY binti Meshack Kambey na Mama Elizabeth Mathayo wa Bunju. Ndoa ni tarehe 22.7.2017.

TANGAZO III

Ndugu ALOYCE NICHOLAUS TARIMO mwana wa Firmini Tarimo na Mama Esterina Mtasiwa toka Parokia ya Kristo Mfalme – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi YVONNE STEVEN MNYANI binti Steven Mnyani na Mama Grace Vedasto toka Parokia ya Mbezi Beach. Ndoa ni tarehe 16/9/2017.

Ndugu MATELULA mwana wa John Matelula na Mama Demetria Florian toka parokia ya Makuburi, anatarajia kufunga ndoa na Bi HELENA binti Chrispin Mdimi na Mama Dolores Mluge toka Parokia ya Makuburi. Ndoa ni tarehe 16/9/2017.

Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hizi atoe taarifa ofisini kwa Paroko.

“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”

Page 1 of 6