ensw

Vicar

Vicar

Hide Main content block

Jumapili Hii

Parokia ya Upanga

 • Historia yetu
  Historia yetu

  Parokia ya Upanga ilizinduliwa rasmi na Muadhama Kardinali Laurian Rugambwa mwaka 1971. Kabla ya hapo ilikiwa kanisa dogo (Chaplaincy) la jumuiya ya Waitaliani waliokuwa wakiishi mjini Dar es salaam.

 • Jumuiya
  Jumuiya

  Jumuiya ya Mlima Yuda Thadei inawaunganisha Wana parokia wanaoishi Mtaa wa Mtitu, Mtaa wa Longido Rangi Barabara ya Umoja wa Mataifa. Jumuiya mmojawapo wanajumuiya takribani 20,

 • Vyama vya Kitume
  Vyama vya Kitume

  Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) ni chama cha kitume cha vijana wa Parokia yetu. Vijana wapo hai na mara kwa mara hukutana kwa ajili ya mafundisho mbali mbali ya imani.que sed bibendum velit.

MAFUNZO

Media type
26:32
283 - Tanzania: If you educate the women, you can educate the village
283 - Tanzania: If you educate the women...
Details
Invited: Cardinal Polycarp PengoNearly 30% of Tanzania's 36 million are Catholic...
Media type
1:11
Pope Francis meets with bishops of Tanzania during their \'ad limina\' visit
Pope Francis meets with bishops of Tanza...
Details
On Friday morning, Pope Francis welcomed members from the Tanzania Episcopal Con...
Media type
6:14
YESU NI MWEMA. Kwaya ya mt. Kizito Makuburi. ( by B. Mukasa).wmv
YESU NI MWEMA. Kwaya ya mt. Kizito Makub...
Details
St. Kizito choir, Makuburi catholic Parish, Dar es Salaam, Tanzania.

Habari Mpya

cache/resized/c211c876767225554f3c74acb8cf4562.jpg 12
August 2015

Tumwombe Mungu kwa ajili ya ndugu yetu Marehemu Mario Maccarini

Ndugu Mario Maccarini ni Mmisionari wa Shirika la Ndugu Wafransisko Wakapuchini kutoka Italia, katika Parokia ya Castiglione, Jimbo la Arrezo. ...

Matangazo

 • MATANGAZO DOMINIKA YA 21 YA MWAKA ‘A’ TAREHE 27/08/2017.
  MATANGAZO DOMINIKA YA 21 YA MWAKA ‘A’ TAREHE 27/08/2017.
  1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Kuaga; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Msamaria mwema.
  1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
  1. KIPAIMARA 2017: 1) Siku ya Kipaimara hapa parokiani ni Jumapil ijayo tarehe 3 September 2017. Kipaimara kitatolewa katika Misa ya saa 4.00 asubuhi. Baba Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo atatoa Sakramenti hiyo ya Kipaimara. Tunawaomba wote tushirikiane katika maandalizi hayo.

  2) Maandalizi ya kiroho ya Wanakipaimara, Wazazi na Wasimamizi yakutakuwa tarehe 2 Septemba 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi. Tunawaomba wote wafike bila kukosa.

  1. TANGAZO LA SEMINA YA MALEZI NA FAMILIA:

  Kamati ya Malezi na Familia ya Halmashauri ya walei Parokia ikishirikiana na baba Paroko na Jimbo Kuu la Dar es Salaam inawatangazia waamini wote kuwa kutakuwa na semina ya malezi na Familia itakayoendeshwa hapa Parokiani siku za Jumamosi kuanzia tarehe 9/9/2017. Semina itakuwa ni ya masaa 2 kuanzia saa 9 mchana kwa muda wa miezi 3. Semina ni kwa ajili ya wanandoa wachanga, wale walioandikisha ndoa parokiani hapa na wachumba. Hata hivyo wote tunakaribishwa kwani malezi na familia ni suala linalohusu jamii yote. Tunawaalika hata wale waliohudhuria semina iliyopita lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza uhudhuria yote. Tunaweza kuwaalika hata wale ambao hawaishi kwenye maeneo ya Parokia yetu.

  1. TOKA JUMUIYA YA MT. IMAKULATA: Jumapili ya leo Jumuiya ya Mt. Imakulata wanauza chai na vitafunwa kila baada ya Misa. Mapato yatatumika kwa ajii ya matendo ya huruma. Wote tunaalikwa kuwaunga mkono.
  1. TOKA JUMUIYA YA MT. YUDA THADEI: JUMBLE SALE!!

  Jumuiya ya Mt. Yuda Thadei, kwa mara nyingine inakualika kwenye Jumble Sale itakayofanyika siku za Tarehe 09 na 10 September 2017 kuanzia saa mbili asubuhi. Jumble Sale itafanyika nyumba na 412, Barabara ya Umoja wa Mataifa (kwa familia ya Mwenda, pale kwenye Keki). Jumble Sale ni nafasi ya pekee sana kupata vitu vizuri sana kwa bei nafuu kuliko kawaida. Karibuni sana, karibuni wote.

  1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru jumuiya ya Mt. Yuda Thadei kwa kutuchangia kiasi cha shilingi laki moja baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita.

  2) Leo mara baada ya Misa ya tatu vijana tutakuwa na ibada ya kuabudu EKARISTI TAKATIFU. Vijana wote mnakaribishwa.

  3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda B na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda C. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

  1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya MAGDALENA WA CANOSSA. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Petro. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
  1. KUAGA: Tunamuaga Paroko msaidizi Fr. Augustine Olomy ambaye amepata uhamisho kuhamia Parokia ya Mbagala Kizuiani hapa Dar es Salaam. Tunamshukuru kwa utume wake katika Parokia ya Upanga. Tunamtakia baraka katika utume wake mpya. Pia tunamuaga Br. Salvatory Nkalango ambaye amepata uhamisho wa kwenda kwenye nyumba yetu kuu – Msimbazi. Tunawatakia wote baraka za Mungu na maisha mema.
  1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I: Ndugu GASPER RICHARD ABDALAH mwana wa Richard Abdalah na Mama Anna Solomon wa KKKT Machame – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi PHILIPINA LEONARD LYAKURWA binti Leonard Mshabaa na Mama Donasia Seneli wa Mengwe – Moshi. Ndoa ni tarehe 14/10/2017.

  TANGAZO II:

  Ndugu ISAAC TITUS CHANZI mwana wa Titus Chanzi na Mama Rosemary Chanzi wa Muhimbili, anatarajia kufunga ndoa na Bi DINA SADA NGOSHANI binti Mmadi Ngoshani na Mama Pauline Ngoshani wa Kijitonyama. Ndoa ni tarehe 11/11/2017.

  Ndugu ELIAS mwana wa Zakaria Mabula na Mama Agnes Tindosi wa Mt. Ambros Taghaste, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAZINAEL binti George Mchomvu na Mama Sensia Greyson wa Mt. Ambros Taghaste. Ndoa ni January 2018.

  TANGAZO III

  Ndugu DEOGRATIUS LAZARI mwana wa Lazaro Ndesingo (sasa marehemu) na MamaAurea Ndesario wa Kilema – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi BORA OMARY binti Omary Hamisa Ndanyungu (sasa marehemu) na Mama Siya Leonard Mkama wa Kigoma. Ndoa ni tarehe 7/10/2017.

  Yeyote mwenye kujua kizuizi cha ndoa hizi atoe taarifa ofisini kwa Paroko.

  “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

 • MATANGAZO ;DOMINIKA YA 20 YA MWAKA ‘A’ TAREHE 20/08/2017.
  MATANGAZO ;DOMINIKA YA 20 YA MWAKA ‘A’ TAREHE 20/08/2017.
  1. MCHANGO WA PILI LEO: Ni kwa ajili ya Ulinzi Parokiani; mchango wa Dominika ijayo ni kwa ajili ya Kuaga.
  1. ROZARI TAKATIFU SIKU YA LEO: Itaanza saa 11.00 jioni. Wote tunakaribishwa.
  1. TANGAZO LA SEMINA YA MALEZI NA FAMILIA:

  Kamati ya Malezi na Familia ya Halmashauri ya walei Parokia ikishirikiana na baba Paroko na Jimbo Kuu la Dar es Salaam inawatangazia waamini wote kuwa kutakuwa na semina ya malezi na Familia itakayoendeshwa hapa Parokiani siku za Jumamosi kuanzia tarehe 9/9/2017. Semina itakuwa ni ya masaa 2 kuanzia saa 9 mchana kwa muda wa miezi 3. Semina ni kwa ajili ya wanandoa wachanga, wale walioandikisha ndoa parokiani hapa na wachumba. Hata hivyo wote tunakaribishwa kwani malezi na familia ni suala linalohusu jamii yote. Tunawaalika hata wale waliohudhuria semina iliyopita lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza uhudhuria yote. Tunaweza kuwaalika hata wale ambao hawaishi kwenye maeneo ya Parokia yetu.

  1. TANGAZO LA WAWATA: Kwa upendo wa Kristo…… Kutakuwa na ziara ya Visiga kwa WAWATA wote wa Jimbo kuu la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utume wetu. Ziara itafanyika tarehe 26/8/2017. Safari itaanza Parokiani saa 12.00 asubuhi. WAWATA wote wanaombwa kuhudhuria kwa kujiandikisha mapema kwa viongozi au kwa Masista. Michango yote imetolewa kupitia Jumuiya, hivyo hakutakuwa na michango mingine ya safari. Tunawatakia utume mwema.
  1. TOKA JUMUIYA YA MT. IMAKULATA: 1) Watakutana leo mara baada ya Misa ya pili kwenye ukumbi wa vijana. Wanajumuiya wote wanahimizwa kushiriki,

  2) Jumapili ijayo Jumuiya ya Mt. Imakulata watauza chai na vitafunwa kila baada ya Misa. Mapato yatatumika kwa ajii ya matendo ya huruma. Wote tunaalikwa kuwaunga mkono.

  1. MATANGAZO YA VIJANA: 1) Tunaishukuru Jumuiya ya Mtakatifu Augustino kwa kutuchangia kiasi cha shilingi elfu 50 baada ya kuwasaidia kufanya usafi Jumamosi iliyopita.

  2) Leo vijana tutaangalia movie ya maisha ya Mtakatifu PIO Yenye mafunzo mbalimbali Vijana wote tunakaribishwa.

  3) Leo katika Misa ya tatu ni zamu ya vijana wa kanda A na wiki ijayo itakuwa ni zamu ya vijana wa kanda B. Mnakumbushwa kuandaa wasomaji wa masomo mapema.

  1. ZAMU YA HUDUMA KANISANI NA USAFI: Jumapili ya leo ni zamu ya Jumuiya ya YUDA THADEY. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt. Magdalena wa Canossa. Tunawakumbusha mchango wa Sh. 30,000/= kwa ajili ya maua.
  1. UHAMISHO: Paroko msaidizi Fr. Augustine Olomy amepata uhamisho kuhamia Parokia ya Kizuiani hapa Dar es Salaam. Tunamshukuru kwa utume wake katika Parokia ya Upanga. Tunamtakia baraka karika utume wake mpya. Pia Br. Salvatory amepata uhamisho wa kwenda kwenye nyumba yetu kuu – Msimbazi. Tutapata nafasi ya kuwaaga rasmi Jumapili ijayo.
  1. KUKARIBISHA: Tunafuraha kumkaribisha Ndugu Baltazar Temu ambaye amejiunga na Jamaa ya Ndugu Wakapuchini – Upanga Parokiani. Tunamkaribisha sana na kumtakia utume mwema.
  1. MATANGAZO YA NDOA: TANGAZO I: Ndugu ISAAC TITUS CHANZI mwana wa Titus Chanzi na Mama Rosemary Chanzi wa Muhimbili, anatarajia kufunga ndoa na Bi DINA SADA NGOSHANI binti Mmadi Ngoshani na Mama Pauline Ngoshani wa Kijitonyama. Ndoa ni tarehe 11/11/2017.

  Ndugu ELIAS mwana wa Zakaria Mabula na Mama Agnes Tindosi wa Mt. Ambros Taghaste, anatarajia kufunga ndoa na Bi HAZINAEL binti George Mchomvu na Mama Sensia Greyson wa Mt. Ambros Taghaste. Ndoa ni January 2018.

  TANGAZO II

  Ndugu DEOGRATIUS LAZARI mwana wa Lazaro Ndesingo (sasa marehemu) na MamaAurea Ndesario wa Kilema – Moshi, anatarajia kufunga ndoa na Bi BORA OMARY binti Omary Hamisa Ndanyungu (sasa marehemu) na Mama Siya Leonard Mkama wa Kigoma. Ndoa ni tarehe 7/10/2017.

  TANGAZO III

  Ndugu JOHN GODFREY RUPIA mwana wa Steven Thomas Rupia na Mama Florah Anitha Rupia wa Anglikana, anatarajia kufunga ndoa na Bi JESSICA MWASARA binti Hussein Yusuf Mwasara na Mama Grace Simon Gumbo wa Upanga. Ndoa ni tarehe 21 October 2017.

  Ndugu AMEDEUS TUKUNJOBA mwana wa Lekha Tukunjoba na Mama Joyce Nchimbi wa Kijichi, anatarajia kufunga ndoa na Bi GLORIA MUNENI binti Angelo Muneni na Mama Godliva Makoko wa Upanga. Ndoa ni tarehe 28/10/2017.

  “Imani yako ni kubwa, na iwe kwako kama utakavyo.”

   

Ratiba za Misa Jumapili

 • Misa ya Kwanza: 7:00am
 • Misa ya Pili: 8:30am
 • Misa ya tatu (misa ya vijana): 10:00am
 • Misa za kati ya wiki: 6:20am

Our Location

 • Katikati ya Mtaa wa Charambe na Barabara ya Umoja wa Mataifa
 • Phone: 123 456 7890 | 123 456 7899
 • Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.